Gossip/Udaku

Wasafi TV rasmi hewani,Diamond afunguka namna ya kuipata

Tarehe April 2, 2018

Diamond akiwa ameshika leseni ya kurusha Matangazo.

Vituo vya Luninga hapa nchini vimepata mpinzani mpya,kufuatia staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuzindua kituo chake cha televisheni.

Akizungumzia kuanza kazi kwa kituo hicho Diamond amesema Wasafi Tv imeanza rasmi leo Aprili 02, 2018 na matangazo yanapatikana kupitia ving’amuzi mbalimbali kikiwemo cha Azam TV.

“Matangazo hayo yameanza kuonekana kuanzia leo na kwa watumiaji wa king’amuzi cha Azam, Wasafi TV itapatikana namba 122.”Amesema Diamond

Kwa upande wa Wasafi Radio,bado haijajulikana itaanza lini rasmi kurusha matangazo yake.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni