Gossip/Udaku

Walichosema Mama Kanumba,Diamond Lulu kuhukumiwa miaka 2

Tarehe November 13, 2017

Diamond katika picha ya pamoja na Lulu.

Hatimaye, baada ya Mwigizaji Lulu kutupwa jela miaka 2,Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kuwa leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipozikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya.

“Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano“Alisema Mama Kanumba

“Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani”  Mama Kanumba

Kwa upande wake Diamond kupitia Istagram amesema “Mwenyezi Mungu ameamua kukupa mtihani huu wewe kwa sababu anaamini wewe ni shujaa na imara…pia anaamini wewe ndio msichana pekee unayeweza kuuhimili mtihani huu… hivyo usisononeke, Make him Proud.”

Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni