Gossip/Udaku

Steve Nyerere avunja ukimya kuwa na ‘bifu’ na Wema Sepetu

Tarehe November 8, 2017

Steve Nyerere akiwa na Wema Sepetu.

Staa wa filamu bongo Steve Nyerere  amevunja ukimya na kudai kwamba hana tatizo lolote na malkia wa filamu Bongo Wema Sepetu.

Inadaiwa kuwa wawili hao kwa muda mrefu wamekuwa hawana mawasiliano mazuri kufuatia Wema Sepetu kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).

“Hatuwezi kuacha urafiki na Wema coz Wema ni dada, ni mtu ambaye tume hangaika naye kuhakikisha kwamba tumafika hapa tulipo na mimi nataka kusema Wema ni mzalendo wa taifa la Tanzania,” amesema Steve

Steve amesisitiza kuwa haina haja ya kutokuwa na mawasiliano  mazuri na Wema kwa kuwa wote ni binadamu hajui kesho nani atamzika.
 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni