Gossip/Udaku

Shamsa Ford amuonya Wema Sepetu kuhama vyama

Tarehe December 6, 2017

Mwigizaji wa filamu za Kibongo Shamsa Ford.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo Shamsa Ford  ametoa  ya  moyoni  kuhusiana na kitendo cha msanii mwezake wa filamu Wema Sepetu kuhama vyama kutoka CCM kwenda Chadema.

Shamsa  amesema hama hama vyama  inawezekana anapata faida lakini cha muhimu asisahau kazi yake.

“Siwezi kuzungumzia sana suala la Wema kuhama vyama maana ni lake binafsi na huenda lina faida kwake, nawasihi tu wenzangu wasisahau kazi yao ya sanaa iliyowatambulisha kwa jamii,” alisema Shamsa.

Ameongeza kuwa   wao siyo wanasiasa hivyo suala la Wema kwenda na kurudi kwenye vyama vya siasa inawezekana.

Mwigizaji Wema Sepetu  alitangaza kuhama kutoka CCM  kwenda Chadema mwezi februari mwaka huu akidai kuwa haridhiki na mwenendo wa Chama hicho.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni