Gossip/Udaku

Shamsa Ford amfunda Shilole

Tarehe December 12, 2017

Ashraf Uchebe akiwa na mkewe, Shilole.

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amemfunda msanii mwenzake wa filamu Shilole mara baada ya kuolewa na mpenzi wake maarufu kama Uchebe hivi karibuni.

Shamsa amempongeza Shilole kwa uamuzi wake wa kuolewa na kumtaka atulie kwenye ndoa yake.

“Hongera sana mamy. Umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.Cha muhimu uwe mke bora wa kitanzania kwa mumeo na ustar uweke pembeni. Mumuweke Mungu mbele, uvumilivu na kuheshimiana Inshaallah mtazikana. Karibu kwenye Chama mama” aliandika Shamsa Ford

Kwa upande wa wasichana wanaosubiri matajiri Shamsa amesema,

Sasa nyie mnao subili matajiri wawaoe wakati hao matajiri wana wake zao wameanza nao moja mtasubili sana mpaka uso uote sugu. Uzuri na Ustar una mwisho wake, itafika muda hata inzi hakusogelei” 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni