Gossip/Udaku

Sasa Tv yamuibua Kiwewe,afichua uhusiano wake na Matumaini

Tarehe June 16, 2017

Screen Shot 2017-06-16 at 9.16.24 AM

Matumaini                                                                                Kiwewe

Msanii wa filamu za vichekesho nchini Tanzania Maarufu Kiwewe aliyetamba na tamthilia ya Baragumu toka katika kundi la Kaole sanaa group, amekanusha uvumi unaoenea katika mitandao ya kijamii kwamba ana mahusiano ya kimapenzi na Matumaini.

Akiongea na hivisasa nyumbani kwake, Kiwewe amesema uhusiano wake yeye na matumaini ni wa kazi pekee siyo mambo mengine.

“Sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na matumaini zaidi ya kushirikiana katika kazi, Hivyo  wanapotosha umma kwani sanaa ilitukutanisha kama mke na mume lakini sio wapenzi nje ya sanaa”Ameongeza Kiwewe.

Kumekuwa na wasanii wengi wanaoendana katika uigizaji kwa nafasi wanazopewa wengi huchukulia kama wana mahusiano  hii imeonekana kwa  Tausi Mdegela, na Mboto au Hemed na Jacline Wolper.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni