Gossip/Udaku

Roma atoa ya moyoni,adai kuishi kwa tahadhari

Tarehe August 11, 2017

roma3

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amefunguka kuwa  baada ya mama watoto wake kumpambania katika matatizo ya kutekwa miezi miwili iliyopita, mashabiki hawataki kuona rapa huyo akimfanyia tendo lolote baya mwanamke huyo.

Rapa huyo amesema kuwa wakati  anapoonekana kupiga picha zenye utata na mwanamke tofauti na mke wake amekuwa akitupiwa maneno ya kashfa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamiii  jambo ambalo linamfanya kuishi kwa tahadhari na umakini mkubwa.

“Natukanwa, nashambuliwa sana tena nikionekana nipo na mwanamke tunatembea maeneo fulani natukanwa sana, wanasema wewe mwanamke wako alivyokupambania halafu unafanya ushenzi,Kwa hiyo inaonekana ni mwanamke fulani aliyebarikiwa na hatakiwi kukosewa kabisa,”alisema Roma.

Hata hivyo rapa huyo amedai kuwa  bado ana  maumivu katika mwili wake hayajapona vizuri hasa kwenye kidole chake kimoja ambacho aliteguka kipindi ambacho alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni