Gossip/Udaku

Range Rover mpya ya Jaguar yawachefua wananchi Kenya

Tarehe February 10, 2018

Wananchi nchini Kenya wanadaiwa kukasirishwa na kitendo cha Mbunge Jaguar kupost picha akipita akiwa na gari lake jipya aina ya Range Rover Sport.

Jaguar alipost picha mtandaoni akiwa karibu na Range Rover Sport mpya, licha ya kuwa hajasema chochote kuhusiana na gari hiyo kama ni yake amenunua au alikuwa anapita karibu ya gari hilo.

Baadhi ya wananchi wamesema  walitegemea kuona mbunge akiwawezesha kununua kilo ya unga na kupata kadi ya kupata matibabu na kuongeza kuwa Wakenya wengi hawawezi kumiliki Range kama hiyo.

“Wewe sio kiongozi tuliyekuchagua tuone unapiga hatua wewe acha kupost vitu facebook na uanze kufanya kazi kwa watu wako waliyokuchagua kuwa kiongozi wao”Alisema Evans Yatich

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni