Gossip/Udaku

Nuh Mziwanda akana kurudiana na Shilole

Tarehe January 11, 2017

nuh-8

Msanii wa muzijki wa kizazi kipya, Nuh Mziwanda, amefunguka na kanusha habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa alikuwa na mpenzi wake wa zamani, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, jijini Mwanza siku mbili zilizopita.

Akizungumza kupitia kipindi Fulani cha lunimga nchini,  Mziwanda amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa alisikia Shilole alikuwa jijini Mwanza kwenye klabu ambayo yeye alikuwa anafanya shoo lakini hawakuonana.

“Mimi siwezi kumkataza mtu kuingia mahali popote, hilo ni jambo la kawaida, niliambiwa yupo humu mjini ‘so’ sikujali maana mimi nilienda kufanya kazi na yeye alikwenda kufanya kazi kimipango yake, kwa hiyo hayo maneno mengine yanayoongeleka mimi mwenyewe siyajui, mimi nimekuja Mwanza kutafuta pesa,” amesema Nuh Mziwanda.

“Mimi nimeoa najiheshimu, siwezi kufanya vitu ambavyo si vya maadili au ambavyo sitakiwi kuvifanya.  Kilichonileta Mwanza ni kufanya shoo na kufanya makubaliano na kusaini mkataba wa shoo yangu nyingine itakayofanyika Dar es Salaam, ” alisisitiza.

Hivi sasa  mwanadada Shilole anatajwa kuendelea kupenda vijana wadogo kwani baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Mtoto Mdogo Mdogo’ alionekana akitoka na ‘kadogoo’ mmoja anayejulikana kwa jina la Hamadai.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni