Gossip/Udaku

Niki wa Pili:’Matukio ya mitandaoni mtaji kwa watawala’

Tarehe December 19, 2017

Mwanamuziki Nikki wa Pili.

Mwanamuzi na Msomi Niki wa Pili amevunja ukimya na  kusema kuwa uwepo wa taarifa nyingi za matukio ya watu maarufu  mitandaoni huwasahaulisha wananchi kuhoji juu ya shida mbalimbali zinazowakabili.

“Sasa hivi ni rahisi kuwasahaulisha watu juu ya ukosefu wa ajira, umaskini, ukosefu wa viongozi nakadhalika, kwa kuwa Media, Social Media kila siku inatupatia utajiri wa taarifa nyingi tukio baada ya tukio. Weusi, Wema, Mange, Dr. Shika, Hamorapa, Meli ya wa china, Trump, Nyimbo mpya, Videos, Karuchi. Utajiri huu wa taarifa na matukio ni jambo jema sana kwa watawala duniani. Na wapigaji wengine ambao ni wananchi tuko bize na taarifa na matukio na bila kujuwa tunakuwa tuna kubaliana na hali ilivyo hakuna pressure wala muda wa kujadili au kupigani ajira, umaskini, Demokrasia, elimu nakadhalika” alindika Niki wa Pili

Nini maoni yako kuhusiana na kauli hii ya Nikki wa Pili?

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni