Gossip/Udaku

Mwakyembe aagiza Nandi akamatwe,Diamond akihojiwa Polisi

Tarehe April 17, 2018

Waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe, amesema msanii Diamond Platnumz alikamatwa jana akidaiwa kusambaza mitandaoni picha zisizo na maadili.

Mwakyembe amesema hayo bungeni leo Aprili 17 na kubainisha kuwa ameagiza msanii mwingine Nandi kusakwa na kukamatwa  kwa tuhuma za kusambaza video ya utupu mitandaoni.

Aidha,Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati anajibu swali la nyongeza la mbunge wa Ulanga Godluck Mlinga aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kukomesha tabia za baadhi ya watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kuhamasisha masuala ya ushoga.

Waziri Mwakyembe amesema serikali imeshatunga sheria inayowabana wasanii na kudhibiti maudhui yasiyo na maadili mitandaoni.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni