Gossip/Udaku

Mongella:’Chanzo cha ubakaji ni wanaume kutojua Kutongoza’

Tarehe September 8, 2017

Getrude

Mwanaharakati mkongwe wa haki za Wanawake na watoto Balozi Getrude Mongella amesema kuwa chanzo cha ongezeko la ubakaji kwa watoto  ni kwa  sababu ya baadhi ya wanaume kuwa waoga na wengine kutojua kutongoza.

Akiongea wakati wa Tamasha la Jinsia linaloendelea kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Balozi Mongella alisema  kama sababu siyo hiyo basi vitendo hivyo vingepungua au kutokuwepo kabisa.

“Hii hali inaumiza, kibaya zaidi wanaoumia ni watoto wetu lakini haya yote ni kwa sababu baadhi yao wameshindwa kutongoza,” alisema Balozi Mongella

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni