Gossip/Udaku

Mkuu wa Wilaya Kinondoni aapa kufa na waliobomoa nyumba ya msanii

Tarehe March 31, 2018

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi amewataka watu waliovunja nyumba ya msanii Mandojo kujisalimisha mara moja.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Ally Hapi amempa  pole  msanii huyo wa muziki wa bongo fleva Man Dojo, na kumtaka afike nyumbani kwake ili aweze kutafuta namna ya kumsaidia.

Hivi karibuni watu ambao hawajajulikana walikwenda nyumbani kwa msanii Mandojo huko Mbweni jijini Dar es salaam, na kuvunja nyumba pamoja na kuiba baadhi ya mali zake.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni