Gossip/Udaku

Mkuu wa mkoa akemea wanafunzi wa kike kuitwa “Baby”

Tarehe November 11, 2017

Baadhi ya wanafunzi katika moja ya shule ya msingi nchini.

Serikali kupitia Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme imepiga marufuku tabia ya wanafunzi wa kike kuitwa “Baby”.

Mndeme amesema hayo katika ziara yake ya siku moja alipotembelea shule ya sekondari Nasuli iliyopo wilayani Namtumbo na kubainisha kuwa tabia ya watoto wa kike kuitwa baby ndio chanzo cha watoto kujiingiza kwenye mapenzi.

“Msikubali kuitwa “Baby” kwasababu kukubali kuitwa “Baby” ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi msikubali kuitwa “Queen” wewe ni mwanafunzi unatafuta maisha”, amesema Mndeme

Mkuu huyo wa mkoa  amewaasa wanafunzi hao kuweka bidii kwenye masomo na kujiepusha na vishawishi ambavyo vinapelekea kupata ujauzito na kulitia hasara taifa ambalo linalipa ada ili wasome bure.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni