Gossip/Udaku

Mdada raia wa Kenya adai kuzaa na Diamond

Tarehe December 8, 2017

Glady anayedai kuzaa na Mwanamuziki Diamond.

Idadi ya wanawake wanaodai kuzaa na Mwanamuziki  Diamond imeongezeka kufuatia mdada mwingine aitwaye Glady  kufika  Tanzania na kudai kuwa amezaa na Diamond.

Akizungumza katika mahoajiano na moja ya chombo cha Habari hapa nchini Glady ambaye ametokea nchini Kenya  amesema alizaa na Mwanamuziki Diamond na mtoto wake ana miezi 7 sasa.

Amesema alikutana ni Diamond Platnumz mwaka 2011 kupitia mtandao wa facebook ambapo walianza mahusiano na hatimaye akampa mimba na , baada ya kubeba mimba hiyo, Diamond alikata mawasiliano.

Kufuatia kukata Mawasiliano  Glady alifika Tanzania kwa mama Diamond na kumweleza hata hivyo mama Diamond alimkataa.

Wakati Glady akijitokeza,miezi kadhaa Mwanamitindo Hamisa Mobeto  naye alijitokeza na kudai kuwa amezaa na Mwanamuziki Diamond ambaye baadae alikubali na kuweka mambo hadharani kupitia vyombo vya habari.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni