Gossip/Udaku

Mbasha afunguka sababu ya kutongozwa na wanawake lukuki

Tarehe October 12, 2017

Mwanamuziki Mbasha.

Mwanamuzi wa gospel nchini Emanuel Mbasha amefunguka kuwa amekuwa akitongozwa na wanawake wa aina mbalimbali tangu aachane na aliyekua mke wake Flora Mbasha.

Akiungumza katika mahojiano na moja ya chombo cha habari hapa jijini Mbasha amesema wanawake wengi wanafunguka hisia za mapenzi juu yake, lakini anamuomba Mungu ampe mtu sahihi zaidi ili yasije yakajirudia yaliyomkuta awali.

Mbasha  ambaye wengi humsifia kwa utanashati wake, amesema anamshukuru Mungu kwa kuonyeshwa kupendwa, baada ya mabinti wengi kumtamani kimapenzi.

“Ukiangalia DM yangu kila siku inajaa meseji, kuna kila aina, na ninamshukuru Mungu kwa kipaji hicho, maana yake kupendwa nako ni kibali na ni baraka za Mungu, sasa nikikurupuka tu kuchukua nitaingia majanga, natamani nipate mtu sahihi, nifanye naye maisha tupate watoto tuendelee mbele,”Alisema Mbasha

Emmanuel Mbasha aliingia katika mgogoro na mke wake Florah Mbasha hivyo ndoa yao kuvunjika, hata hivyo Florah anadaiwa kuolewa na mwanaume mwingine.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni