Gossip/Udaku

Maumivu ya Wastara yamgusa Rais Magufuli, amchangia fedha za matibabu

Tarehe January 27, 2018

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi fedha Wastara.

Ndoto ya Msanii wa filamu Wastara Juma kutibitiwa mguu nje ya nchi sasa itatimia kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mke wake Mama Janet Magufuli kumchangia shilingi milioni 15.

Fedha hizo  Wastara amekabidhiwa na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike , sambamba na kiasi kingine cha milioni moja na laki tisa ambayo ni michango kutoka kwa wasaidizi wa Rais.

Rais Magufuli anakuwa mtu wa kwanza kutoa fedha nyingi kwa msanii huyo, tangu aanze kutoa rai ya kuomba michango, ambapo wiki iliyopita waziri wa Habari, sanaa, michezo na utamaduni Dkt. Harison Mwakyembe alimkabidhi shilingi milioni moja.

Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na mguu kwa muda mrefu na alikuwa kaomba msaada wa watanzania mitandaoni ili aweze kwenda nchini India kupatiwa matibabu.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni