Gossip/Udaku

Mama Dogo Janja afunguka alivyoshiriki ndoa ya mwanae na Uwoya

Tarehe November 2, 2017

Dogo Janja akiwa na mama yake.

Mama mzazi wa msanii Dogo Janja Bi. Zaituni Omari,  kwa mara ya kwanza amefunguka na kusema kuwa  alimpa baraka zote ili mwanae amuoe Irene Uwoya.

“Alishawahi kuniambia kuwa anataka kuoa na mimi nikampa baraka zote, alivyokuwa tayari alinijulisha akaniambia kama kuna uwezekano niende isipokuwa kuna mambo yakaingilia kati, ila kwa vile Madee ni kama baba yake na ninamuamini sana nikawaruhusu waendelee, kila anachofanya hafanyi yeye kama yeye lazima kiko nyuma yangu, sio stori za kiki ni kweli kaoa” Amesisitiza mama Dogo Janja.

“Nimeridhika kwa sababu hata dini yetu ya Kiislam Mtume Mohamad alioa mwanamke mkubwa, kwa hiyo umri haujalishi, kikubwa na maelewano”, ameongeza  Mama yake Dogo Janja.

Hata hivyo ndoa hiyo imezua gumzo nchini kufuatia tofauti kubwa ya umri wa mwanamuziki Dogo Janja na muigizaji wa filamu za kibongo Irene Uwoya.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni