Gossip/Udaku

Madai ya kuwashambulia ‘shilawadu’ yamuibua Mose Iyobo

Tarehe February 5, 2018

Mose Iyobo akiwa na mama wa mtoto wake.

Madai ya watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kushambuliwa na Dansa wa kundi la Wasafi Classic (WCB), Mose Iyobo yamemuibua  dansa huyo na kukana vikali kitendo hicho.

Iyobo  amesema  madai ya kuwashambulia watangazaji hao na wafanyakazi wengine wa televisheni hiyo ameyasikia kwenye mitandao ya kijamii na katika kipindi hicho.

“Nimesikia kupitia kipindi chao na kwenye mitandao ya kijamii, sina nguvu hiyo, mimi si baunsa wala mkorofi”Amesema Iyobo

Mapema  Februari 2, 2018  watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kupitia mitandao ya kijamii na kipindi hicho walieleza kushambuliwa na Iyobo ambaye ni mpenzi wa mwigizaji Aunt Ezekiel.

“Usiku wa leo wakati tukiwa kazini tumenusurika kumwagwa damu na mtu tuliyemfuata kumuomba mahojiano, kati yetu kuna walioumia viuno na  mikono, pia  kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi.”Walisema Watangazaji hao.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni