Gossip/Udaku

Joh Makini asema muda ukifika ataachia albamu

Tarehe January 11, 2017

johm20akini20

Msanii wa muziki nchini Joh Makini amefunguka kuhusiana na  mipango yake wa kuachia albamu yake mwaka huu.

Joh Makini amesema, Kwa sasa wasanii wengi wa muziki Bongo wamekuwa na msukumo mkubwa wa kuachia albamu huku Navy Kenzo wakiwa wamefungua njia hiyo baada ya kufungwa kwa miaka mingi.

Staa huyo  wa Perfect Combo ameongeza kuwa mashabiki watulie kuhusu kolabo zake alizofanya na Falz, Davido na YCEE (wote kutoka Nigeria) watazisikia kwa kuwa amezifanya nyimbo hizo kwa ajili yao.

Rapper huyo amesema, mpaka sasa ana albamu mbili ambazo zipo tayari ila hajajua muda wa kuachia.

“ Mpaka sasa nina albamu mbili, mipango ya kuiachia ipo,nikiwa tayari nitasema,” amesema Joh.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni