Gossip/Udaku

Je Wolper ‘kampiga chini’ rasmi Harmonize au ni kiki tu?

Tarehe January 5, 2017

Wolper na Harmonize

Wolper na Harmonize

Ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Msanii wa Filamu, Jackline Wolper kukanusha vibaya kumpiga chini mpenzi wake Harmonize,  sasa upepo unaonekana kubadilika ukionesha kuwa pengine wawili hao ‘itabaki kuwa stori’.

Dalili zinaonesha kuwa Wolper amembwaga rasmi Harmonize kupitia post aliyoituma katika Instagram yake licha ya post hiyo kukaa muda mfupi tu hewani na kufutwa.

Kwenye post hiyo iliyokuwa na picha ya Harmonize pamoja na emoji za alama ya kopa iliyopasuka, Wolper ameandika: Nina akili timamu me syo mtoto mdogo, endelea na maisha yako it over waambie rasmi usifiche @harmonize_tz i hate love.”

wolper

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni