Gossip/Udaku

Hatimaye Chuchu Hans ajifungua mtoto wa kiume

Tarehe January 12, 2017

4ee96-chuchunaray

Msanii  wa filamu Bongo, Chuchu Hans, hatimaye amejifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Chuchu ni mwanamke wa kwanza kumpatia muigizaji mkubwa wa kiume Vincent Kigosi ‘Ray’, mtoto.

Ndugu wa karibu na mastaa hao alithibitisha kujifungua kwa Chuchu na kusema kuwa ujio wa mtoto huyo ambaye wamempa jina la kwanza la Vincent Junior, kuwa ameleta furaha kubwa kwa  Ray.

“Yaani Ray, alikuwa Zanzibar kwa ajili ya kungalia mpira lakini alipopata habari hiyo alionekana mwenye furaha sana huku baadhi ya mastaa wenzake wakimpongeza,” amesema ndugu  huyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni