Gossip/Udaku

Harmonize ajiweka pembeni,Zari kumbwaga Diamond

Tarehe April 7, 2018

Zari akiwa na Harmonize.

Mwanamuziki kutoka WCB Harmonize ametoa ya moyoni kufuatia kuvunjika kwa Mahusiano ya Zari na Diamond Platnumz.

Akizungumza katika mahojiano na moja ya Chombo cha Habari hapa nchini Harmonize amesema kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa sababu yale ni maamuzi yake binafsi.

“Mimi naheshimu sana maamuzi ya mtu siwezi kuongea kama ni vibaya au ni vizuri Kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu Mahusiano Yake ndio sina”.

Miezi miwili iliyopita siku ya wapendanao Zari alitumia ukursa wake wa Instagram kumwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond. Uamuzi wa Zari unafuatia Diamond kudaiwa  kuzaa na Mlimbwende Hamisa Mobeto.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni