Gossip/Udaku

Fid Q: kizazi cha digitali kimemezwa na matumizi ya ‘Internet’

Tarehe September 4, 2017

Mwanamuziki Fid Q.

Mwanamuziki Fid Q.

Msanii wa hip hop bongo Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q, amesema anasikitishwa na hatama ya maisha ya kizazi cha sasa kwani kimeharibiwa kwa kiasi kikubwa na mitandao.

Fid Q amesema kizazi cha sasa hakina muda kabisa wa kujisomea vitabu ili waweze kujiongezea ujuzi, kwani mabadiliko ya teknolojia yamechukua sehemu kubwa ya maisha yao.

“Nawaonea huruma sana watoto wa kizazi hichi, mtu anatoka mapumziko anakutana na stori ya Alikiba katoa fresh remix, itamvuruga kabisa kwenda kuzingatia somo la hesabu ambalo linafuatia, sijui tunafanyaje lakini nawaonea huruma sana, sababu mi ni zao la analojia”, alisema Fid Q.

Kizazi cha vijana wa sasa kimeharibikiwa na masuala ya Internet ambapo hutumia mwingi kwenye internet kufuatilia masuala yasiyo na tija katika maisha yao.

Elimu ya jinsi ya kutumia mitando ya kijamii kwa manufaa chanya inahitajika ili kuokoa kizazi cha sasa.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni