Gossip/Udaku

Ebitoke afunguka ‘wanaomsakama’ kuhusu Ben Pol

Tarehe June 16, 2017

_DSC0266

Msanii wa vichekesho nchini Tanzania toka kampuni ya Timamu Afirican Media  anayefanya vizuri kwa sasa  amefunguka na kusema amebadili muonekano wake kwa ajiri ya Ben Pol.

Akiongea na Mtandao huu Nyumbani kwake,Ebitoke amesema nafsi yake inampenda  Ben pol na anaamini ipo siku atampata tu na kuwa mumewe wa ndoa.

“Watu wananitukana sana kuhusu muonekano wangu hivyo nimewaonesha kuwa mimi ni mzuri na hakuna atakayenisababisha niache kumpenda Mgogo wangu” amesema Ebitoke

Hali hii imezidi kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii tangu Ebitoke aseme wazi kuwa anampenda Ben Pol na yupo tayari kuolewa nae.

“Nawaomba mashabiki wangu watambue kuwa kuna maisha nje ya kazi ya sanaa hivyo waheshimu hisia zangu  na waamini nampenda Ben Pol katika maisha yangu.”Alisisitiza Ebitoke.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni