Gossip/Udaku

Dudu Baya adai ajafulia kama watu wanavyodai

Tarehe January 12, 2017

Dudu-Baya

Msanii mkongwe wa muziki nchini wa hip hop, Dudu Baya amesema  ukimya wake kwenye muziki umesababishwa na kuwa busy kwenye biashara na siyo kwamba amefulia kama baadhi ya watu wanavyodai.

Staa huyo wa rapper  amesema  kwa sasa maisha yake yako Mwanza na Kampala akija Dar anakuja kufanya kazi za kisanaa japo alishaamua kupotezea muziki na kufanya biashara zake mbalimbali kwa kuwa haishi kwa kutegemea muziki pekee.

“Sijafulia kama watu wanavyodhani mimi na biashara zangu nyingine na muda mwingi sipo Dar es Salaam. Watanzania ndiyo tabia yao hiyo wakiona msanii haonekani wanadhani amefulia mfano watu walipoona King Crazy GK amepotea walidhani amefulia kumbe alikuwa chimbo anapiga kitabu na saizi tayari ana masters yake” amesema  Dudu Baya.

Dudu Baya amesema ,kauli ya Darasa kuimba kwamba ‘siyo chui, simba wala mamba ngozi yake inamtosha kujigamba’ haijamsumbua kwa kuwa Darasa ni kijana wake na ni msanii ambaye amepambana kwa muda mrefu ila kwa sasa kafanikiwa hivyo anampongeza kwa mafanikio.

Rapper huyo alikuwa akifanya vizuri na kibao chake cha ‘nakupenda mpenzi’.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni