Gossip/Udaku

Dogo Janja ajiita ‘mfalme’ wa kupiga pamba

Tarehe June 12, 2017

Mwanamuziki Dogo Janja.

Mwanamuziki Dogo Janja.

Msanii wa muziki a kizazi kipya nchini Tanzania Dogo Janja anayetamba kwa ngoma My Life, na kidebe amefunguka na kusema kwa sasa hakuna msamii anayejua kuvaa zaidi yake.

Akiongea na kituo kimoja cha radio ,Janja amesema pengine watasema natafuta kiki la hasha huo ndio ukweli wa mambo na kama yupo ambaye anahisi anaweza kushindana nami ajipange.

“Mie sitegemei masoko ya ndani mzigo wangu naagiza toka nje hivyo nakuwa tofauti na wanaonunua hapa ndani maana inakuwa ni sare ya jiji”amesema

Hali hiyo iliwahi kujitokeza mwanzo kwa msanii Jux aliyekuwa anaonekana kuwafunika wasanii wote kwa kuvaa licha ya kuwa wapo waliosema hajui kuvaa.

Rapper huyo alisisitiza kuwa heshima ya msanii inakuja pamoja na mwonekano wake, Hivyo wasanii wanatakiwa kuwa tofauti na mashabiki kwa kuvaa mavazi yenye muonekano  tofauti.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni