Gossip/Udaku

Diamond,Mobeto wafikia pabaya

Tarehe October 7, 2017

Mobetto,Diamond Platnumz.

Mapenzi kati ya Mwanamuziki Diamond na Hamisa Mobeto yanadaiwa kufikia pabaya kufuatia Mobeto kufungua kesi Mahakani dhidi ya Diamond kwa kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.

Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili Zulu mapema wiki  hii   amesema mteja wao Hamisa Mobeto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa rasmi  Oktoba 30, mwaka huu.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni