Gossip/Udaku

Diamond aeleza mchango wa Wema kwenye Chibu Perfume

Tarehe June 13, 2017

Wema-na-Diamond-1 (1)

Msanii wa muziki, Diamond platnumz amefunguka na kuweka wazi juu ya mchango wa malkia wa filamu, Wema Sepetu kwenye perfume yake ya ‘Chibu Perfume’.

Diamond alikiambia kimbindi Fulani cha redio alipokuwa akifanya mahojian kuwa, yeye na Wema wanakutana na kuongea sana na wakati mwingine hushauriwa mambo mengi ya kibiashara na mwanadada huyo ambae alikuwa mpenzi wake .

“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana wakati mwingine tunakutana tu sana lakini sio kwenye media. Tushakuwa kila mtu ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake hata ukiangalia katika Perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alilitoa Wema” alisema Diamond.

Muimbaji huyo kwasasa yupo kwenye mahusiano ya Zari na tayari wamefanikiwa kupata watoto wawili Tifaa na Nillan.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni