Gossip/Udaku

Ben Pol amshauri Producer Sappy kufanya kazi

Tarehe January 10, 2017

ben-paul1

Msanii wa muziki nchini Ben Pol  amefunguka na kumtaka  Producer Sappy kufanya kazi kuliko kutengeneza maneno.

Ben Pol anaonesha kumshangaa Sappy kwa kitendo cha kusema amewachukulia wimbo wao wakati sivyo.

“Unajua sijaelewa kabisa hii issue ilivyokaa kwa sababu huu wimbo nimeandika neno moja moja,” amesema  Ben.

Mkali huyo wa Phone amefananisha kitendo hicho kama kujenga nyumba yako inaisha halafu baadaye anatokea mtu anasema nyumba ni yake, alipoulizwa kwanini Sappy kaamua kufanya hivyo Ben Pol amesema, “Labda anataka aonekane, afanye kazi ataonekana haina haja ya kutengeneza drama.”

Kwa upande mwingine, Ben Pol amesema tarajia album kutoka kwake ambayo itatoka mwezi ujao (February) ikiwa na ngoma 12 ikiwepo Moyo Mashine Remix ft Chidnma, Phone ft Mr Eazi, Natuliza Boli, Bozimba ft Chidnma.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni