Gossip/Udaku

Aika akerwa na wanaosambaza nyimbo za albamu yao mpya

Tarehe January 10, 2017

navy-kenzo-aim-album-art

Msanii wa muziki nchini kutoka katika Kundi la Navy Kenzo, Aika ameonyeshwa kuhudhunishwa na kuvunjwa moyo na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakizivujisha nyimbo kutoka kwenye albamu yao mpya ‘AIM’ na kuzisambaza mitandaoni.

Aika amesema,  kitendo cha baadhi ya watu hususani bloggers kuchukua nyimbo hizo kwenye albumu na kuziweka mitandaoni kinakuwa kinawavunja moyo kwani kinasababisha biashara yao kupunguza kasi na kuharibu mauzo ya album hiyo mtaani.

“Inasikitisha sana pale msanii unapofanya kitu kikubwa halafu baadaye mtu anaitoa bure kazi yako, sisi kama Navy Kenzo tumefanya kazi kubwa sana mpaka kukamilisha hiyo kazi, tumethubutu, sasa unapoona blogs zinaweka zinatuharibia biashara hata watu wanaonunua albamu wakiona tena mtandaoni wanajisikiaje,” amesema Aika.

Muimbaji huyo alisisitiza kuwa anatambua bloggers huenda wanajua wana wa’support’ kwa ku-upload nyimbo hizo kwenye mitandao ya jamii ili kusaidia albumu kuuzika lakini huenda wengine hawajui kile wanachofanya kinawaharibia wao soko la albumu yao mtaani.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni