Sheria na Mahakama

Yeriko Nyerere apandishwa kizimbani kwa makosa ya mtandaoni

Tarehe June 2, 2017

1

Mfanyabiashara Yericko Nyerere leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook.

Wakili wa Serikali, Elia Athanas amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao Namba 14 ya 2015.

Kesi hiyo namba 184 ya 2017 imeahirishwa hadi Juni 5 ambapo mshtakiwa huyo atasomewa maelezo ya awali (PH) na yupo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Shilingi Milioni 10.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni