Sheria na Mahakama

Mtunza bustani kizimbani kwa kumtusi Rais Magufuli na Makamu wake

Tarehe January 10, 2017

dsc_1186

Mtunza bustani Maganga Masele, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu utendaji wao wakuliongoza taifa.

Wakili wa Serikali Lucy Mallya amesema kuwa Desemba 22, mwaka jana Masele akiwa Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es salaam, alitoa lugha ya matusi dhidi ya Rais Magufuli na Samia, maneno ambayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo, Masele alikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo Mallya alidai kuwa upelelezi haujakamilika pia hakuna pingamizi la dhamana kwa kuwa kisheria kosa hilo linadhaminika.

Kwa upande wake Hakimu Mwijage amesema kuwa ili mshitakiwa awe nje kwa dhamana ni lazima awe na mdhamini  mwenye barua yenye utambulisho atakayesaini bondi ya shilingi 500,000.

Masele alikamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana hadi Januari 24, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni