Sheria na Mahakama

Mhasibu tajiri wa Takukuru apandishwa kizimbani kwa mashtaka 43

Tarehe November 17, 2017

Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Godfrey Gugai, na Maafisa wengine watatu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na kusomewa mashtaka 43.

Mbele ya Hakimu Mkazi Kiongozi Thomas Simba, Gugai amesomewa mashtaka tofauti yakiwemo ya kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutakatisha fedha na kudanganya mali anazomiliki.

TAKUKURU imemfikisha mahakamani, Gugai kwa tuhuma za kumiliki mali nyingi ambazo haziendani na kipato chake jambo ambalo ni kunyume cha sheria ya Utumishi wa Umma.

Hatua hii imekuja baada ya siku chache zilizopita, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Generali, John Julius Mbungo, alitangaza dau nono la shilingi milioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa Godfrey Gugai, ambaye hakuwa anajulikana alipo, lakini Novemba 15, alijisalimisha mwenyewe na kuhojiwa na taasisi hiyo.

Mali zilizotajwa kumilikiwa na Gugai ni pamoja na viwanja zaidi ya 30, magari matano, nyumba 5 na piki piki moja ambavyo vitu hivyo viko maeneo mbalimbali hapa nchini.

Mtuhumiwa huyo na wenzake wapo rumande baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 4, mwaka huu.

Miongoni mwa mali anazodaiwa kumiliki ni kama ifuatavyo;

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni