Sheria na Mahakama

Manji agonga Mwamba Mahakama Kuu, amkataa wakili wa Chadema

Tarehe August 7, 2017

manji-7

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya dhamana ya mfayabiashara Yusufu Manji anayekabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi.

Jaji Isaya amefikia uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja za upande wa Serikali kufuatia mfanyabiashara huyo kupeleka maombi ya kupata dhamana.

Wakati huohuo, Manji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala (CCM) amekataa kendelea kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa madai kuwa wakili huyo ni wa Chadema wakati yeye ni Mwanachama na Diwani wa CCM.

Amesema alipopeleka maombi ya dhamana Mahakamani hapo, alimpa maelekezo Wakili Joseph Tedayo lakini alishangaa kesi ilipoitwa kwa ajili ya kusikilizwa, akawakilishwa na Wakili Kibatala.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni