Sheria na Mahakama

Manji aachiwa huru kesi ya Dawa za Kulevya

Tarehe October 6, 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya Dawa za Kulevya iliyokuwa ikimkabili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Hukumu hiyo imetolewa leo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya na kufanya kuwa kesi ya pili kwa mfanyabiashara huyo kuachiwa huru ndani ya kipindi kifupi baada ya Mwendesha Mashtaka (DPP) kuamua kutoendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili ya uhujumu uchumi hivi karibuni.

Katika kesi hiyo, Manji alikuwa anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga Wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.

Hatahivyo katika utetezi wake, Mfanyabiashara huyo alidai kuwa ana matatizo ya moyo ya kurithi kutoka kwa babu zake na alianza kuugua akiwa na miaka 26 na amekuwa akitumia madawa hayo kama sehemu ya tiba kwake.

Awali, ushahidi wa upande wa utetezi  mahakamani hapo ulionesha kuwa Manji ana vyuma katika moyo wake.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni