Sheria na Mahakama

Malima aburuzwa mahakamani kwa kosa la shambulio

Tarehe May 16, 2017

Adam Malima.

Adam Malima.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Adam Kighoma Malima pamoja na dereva wake leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya shambulio na kuzuia askari polisi kufanya kazi yake.

Akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amedai kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi Malima alimzuia Ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake halali ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.

Naye mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani Mohammed Kigwande anakabiliwa na shtaka la kumshambulia Mwita Joseph.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa akiwa na nia ya kumzuia Mwita Joseph ambaye ni Ofisa Oparesheni wa Kampuni ya Priscane Business Enterprise wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL, alimshambulia Mwita na kumsababishia maumivu.

Washtakiwa hao wanaotetewa na Wakili Peter Kibatala wamekana shtaka dhidi yao ambapo upande wa Jamhuri umedia kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kila mmoja kuwa na mdhamini ambaye atasaini bondi ya Shilingi milioni tano.

Kesi hiyo namba 168 ya 2017 itatajwa tena Juni 15, mwaka huu ambapo pia pingamizi la upande wa utetezi litasikilizwa baada ya Wakili Peter Kibatala hapo awali kuwasilisha pingamizi dhidi ya shtaka la pili kwa madai kuwa halifanani na maelezo ya kosa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni