Sheria na Mahakama

Mahakimu waaswa kuzingatia haki ya dhamana

Tarehe December 31, 2016

mahakama

Mahakimu wote nchini wametakiwa kuzingatia sheria katika utendaji wao wa kazi hasa katika utoaji wa dhamana ambayo ni haki ya msingi ya mshtakiwa.

Hayo yamesemwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati Mjini Moshi alipokuwa akizungumza na mahakimu wa ngazi  zote katika mahakama za mjini Moshi baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika mkoa wa Kilimanjaro.

Hata hivyo, Mahakama inaweza kuzuia dhamana endapo kutakuwa na pingamizi la kisheria, na mara nyingi mapingamizi hayo yamekuwa yakiambatana na hati kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na malalamiko dhidi ya baadhi ya mahakimu kuwanyima dhamana washtakiwa ilhali mashtaka yao yanaruhusu kupata dhamana hasa malalamiko kutoka kwa mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakipambana ili mteja wao apate dhamana baada ya kukwaa kisiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Bernard Mpepo ilisema msajili huyo amewataka mahakimu watunze maadili yao ili kujenga imani kwa jamii.

Msajili Mkuu pia alitembelea Gereza Kuu la Karanga mjini Moshi na kufanya ukaguzi wa kawaida na kisha kuzungumza na wafungwa, mahabusi na wafanyakazi wa gereza.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni