Sheria na Mahakama

Mahakama yakataa ombi la Manji kwenda kuhojiwa na TRA

Tarehe August 9, 2017

Mfanyabiashara Yusuph Manji alipofikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetupilia mbali maombi ya upande wa mashtaka ya kutaka Mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji kuhojiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu masuala ya kodi.

Maombi ya kutaka Manji ahojiwe na TRA, yaliwasilishwa mapema leo asubuhi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa ambaye aliiomba Mahakamani itoe kibali ili mtuhumiwa huyo akahojiwe na kisha arudishwe kabla ya muda wa kazi haujaisha.

Kabla ya uamuzi wa mahakama, Wakili wa Manji, Alex Mgongolwa alidai kuwa ombi hilo sio sahihi kwakuwa walikwishafanya mawasiliano ya maandishi na TRA na kwamba wapo mawakili wa Manji wanaoshughulikia masuala hayo ya kodi, na hivyo wanapaswa kuwasiliana nao ili mahojiano hayo yawe na manufaa.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkeha amesema kuwa hawezi kuruhusu ombi hilo kwasababu kesi iliyopo mbele yake ni ya uhujumu uchumi ambayo haihusiani na masuala ya kodi na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni