Sheria na Mahakama

Kigogo UVCCM Arusha apandishwa kizimbani

Tarehe August 12, 2017

20728347_1550993391610740_6752064591741646879_n

Mahakama ya Hakimu Mkazi, Arusha imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Vijijini.

Miongoni mwa makosa aliyosomewa mahakamani hapo ni pamoja na kutuhumiwa kujifanya Afisa Mtumishi wa Serikali (TISS) huku kosa lingine likiwa ni kugushi moja ya nyaraka za serikali (kitambulisho).

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Penina Joakim amesema kuwa mnamo Mei 18 katika hotel ya Skyway iliyopo Makao Mapya Jijini Arusha, mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa Utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya utapeli .

Wakili Penina ametaja kosa la pili ambalo Lengai anatuhumiwa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya Kikosi Maalumu Agent (undercover) chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria.

Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana hadi pale kesi yake itakapotajwa tena.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni