Sheria na Mahakama

Kesi ya Aveva, Kaburu yapigwa kalenda, warudi rumande

Tarehe August 7, 2017

DGnLeakXcAADwUm

Kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili Rais wa Simba, Evance Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imeahirishwa hadi Agosti 16, mwaka huu.

Viongozi hao ambao wapo rumande hadi sasa walifika Mahakama ya Kisutu leo kwa ajili ya kutajwa kwa kesi yao ambapo upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodaiwa kuonyesha kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni watuhumiwa hao kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 (Zaidi ya shilingi milioni 700 za kitanzania).

Shitaka lingine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, na la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, ambapo inadaiwa Aveva na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.

Shitaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya  Barclays Tawi la Mikocheni Jijini Dar es Salaam, na la tano ni la kutakatisha fedha tena, likimhusu Makamu wa Rais, Kaburu anayedaiwa kumsadia Aveva kutakatisha fedha katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.

DGnLeakXcAADwUm DGnLeajXcAACaYu

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni