Sheria na Mahakama

Hatima ya Lulu kujulikana Novemba 13

Tarehe October 27, 2017

Washauri watatu wa Mahakama kuu wamesema mshitakiwa Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia, aliua bila ya kukusudia.

Washauri hao wamesema hayo mapema jana wakati kesi hiyo iliposikilizwa ambapo hukumu kamili ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa Novemba 13, mwaka huu.

Baada ya kusikiliza maoni ya baraza la wazee Mahakama imesema kuwa Elizabeth Michael amekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia, muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake na hukumu yake itatolewa Novemba 13.

Wazee hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.

Kabla ya  wazee hao kutoa maoni, Jaji Sam Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni hayo.

Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii wa filamu, Steven Kanumba, akidaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu, Sinza Vatican, Jijini Dar es Salaam.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni