Sheria na Mahakama

DPP aachana na Mbunge Lwakatare kesi ya ugaidi

Tarehe August 11, 2017

COURTAPEAL

Mahakama ya Rufaa Tanzania imeyafutilia mbali maombi ya kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kutaka kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kufuta shitaka la ugaidi lililokuwa likimkabili Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare, tangu mwaka 2014.

Maombi hayo yamefutwa leo na Jaji Mussa Kipenka baada ya Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka kudai kuwa DPP ameamua kuondoa kibali cha maombi hayo kwakuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kutoka na hatua hiyo, Lwakatare ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema sasa anakabiliwa na kosa moja la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky kwa kutumia sumu, kesi ambayo inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Awali, Lwakatare na mwenzake, Ludovick Rwezaura walikuwa wakikabiliwa na jumla ya mashtaka manne likiwemo la kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi kwa lengo la kumdhuru kwa sumu aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.

Mashtaka mengine yalikuwa ya ugaidi wakidaiwa kuandaa mikutano ya kupanga makosa ya kigaidi na kufadhili vitendo vya kigaidi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni