Sheria na Mahakama

Bob Wangwe ahukumiwa jela mwaka na nusu au faini milioni 5 makosa mtandaoni

Tarehe November 15, 2017

Mtoto wa marehemu Chacha Wangwe, Bob Wangwe leo amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela au faini ya Shilingi Milioni 5 baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya mtandao.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akikabiliwa na makosa ya mtandao kufuatia chapisho aliloandika katika ukurasa wake wa Facebook Machi 15, mwaka huu kama ifuatavyo;

“Tanzania ni ambayo…inajaza chuki wananchi matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”

Hatahivyo Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na ndugu wa familia ya Bob Wangwe wanahangaika kulipa faini hiyo ili kumnusuru na kifungo cha jela.

Endelea kuwa nasi kujua hatima ya sakata hili.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni