Sheria na Mahakama

7 kizimbani kwa kumchoma mkulima mkuki mdomoni hadi shingoni

Tarehe December 29, 2016

Mkulima mmoja wa Kitongoji cha Upangwani Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze JImbo la Mikumi Morogoro aliyepigwa mkuki.

Mkulima mmoja wa Kitongoji cha Upangwani Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze JImbo la Mikumi Morogoro aliyepigwa mkuki.

Watu saba kati ya 12 wamepandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumjeruhi kwa kumchoma mkuki mdomoni hadi kutokea shingoni mkulima, Augustino Mtitu,35.

Watuhumiwa hao walipandishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Kilosa huku wengine watano, wote wakazi wa kitongoji cha Upangwa wilayani Kilosa wakisubiri kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, amesema hayo alipokuwa anazungumzia msako uliofanywa na polisi na kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao baada ya kutokea kwa tukio hilo Desemba 25, mwaka huu, majira ya saa tano asubuhi eneo la kitongoji cha Upangwa, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata na Tarafa ya Masanze wilayani Kilosa.

Amesema katika msako huo, watu 12 walikamatwa na saba kati yao tayari wamefikishwa mahakamani. Wengine watano watafikisha mahakamani baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Mbali na Mtitu, amewataja majeruhi wengine wa tukio hilo kuwa ni George Andrew, 68 aliyejeruhiwa kichwani.

Wengine ni Yohana Wisa, 26 aliyejeruhiwa mkono wa kulia, Mathayo Elia, 34 aliyejeruhiwa kichwani na bega la kushoto, Josephat Mtitu, 55, aliyejeruhiwa begani na shavuni na mwingine ni Paulo Thomas, 56 aliyejeruhiwa mbavu na mkono wa kushoto.

Wote ni wakazi wa kijiji cha Dodoma Isanga na wanaendelea vizuri. Hivi karibuni, baadhi ya wafugaji wa jamii ya kimasai waliwashambulia kwa silaha za jadi na kuwajeruhi watu sita akiwemo Mtitu mara baada ya kukamata mifugo ya mtu mmoja aitwaye Ngoyoni Kimang’ati, iliyokuwa ikiharibu mahindi shambani.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni