Mitindo

Zingatia haya kucha zako zisikatike

Tarehe December 22, 2016

images-3

Wanawake na  Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza na husaidia kuondoka na magonjwa yanayotokana na uchafu.

Muda mwingine unakuta mwanamke anakuwa na wakati mgumu wa kuweza kukabiliana na matatizo ya kukatika kwa kucha, kutokana na kusahau masuala kadhaa muhimu wanayopaswa kuzingatia ili kuzipa kucha uimara na afya njema pia.

Kwanza kabisa si vizuri mtu kula kucha zake,kwani  kucha huweza kusababisha kuzikata bila mpangilio maalumu na wakati mwingine husababisha vidonda kwani hula mpaka nyama zinazogusana na kucha.

Tumia glopsi au hata mfuko wa plastiki unaposhika vitu vyenye kemikali, kwani vinaweza kuharibu kucha zako kama dawa za nywele.

Safisha kucha zako mara kwa mara kwa kutumia vifaa maalum wanashauri kusafisha kucha zako kwa kutumia maji ya uvuguvugu na si ya baridi.

Usitumia kucha zako kukwangulia vitu vigumu, kuparua au kuzolea uchafu, hii husababisha kucha zako kukatika vibaya na kuwa na uchafu mweusi usiopendeza.

Usitoe hovyo vinyama vinavyojitokeza pembeni mwa kucha kwani vipo vifaa maalum vya kutolea vinyama hivyo, unashauriwa kutumia vifaa hivyo ili kuziwezesha kucha zako kupumua pamoja na kukuwa vizuri.

Paka rangi kucha zako mara kwa mara kwani wakati mwingine unashauriwa kumechisha rangi ya kucha zako na baadhi ya rangi ya nguo utakazovaa.

Tumia dawa maalumu ya kutoa rangi maarufu kama remover, baada ya kutoa rangi hiyo kwa kiwembeau kitu chenye makali.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni