Mitindo

Uganda yapiga marufuku kufuga kucha na kujipodoa

Tarehe July 8, 2017

mikucha

Kama ulikuwa una ndoto za kufanya kazi nchini Uganda hasa kwa watoto wa kike wenye kupenda kujipodoa na kuvaa nguo zinazoonyesha maumbile basi jua hautaweza kudumu wala kupata kazi nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa edaily wa Kenya, umeripoti kuwa serikali ya Uganda imepiga marufuku uvaaji wa nguo fupi makazini, upakaji make up uliozidi, kubandika kucha ndefu na bandia, kuweka nywele bandia na kuzipaka rangi, kuvaa nguo inayobana kama vile Tshirt na magauni pamoja na kuvaa vivalio.

Miaka 2013 nchi hiyo ilitunga sheria ya kukataza kuvaa nguo fupi, sheria ambayo ilizua mijadala nchini humo na sehemu zingine.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni