Mitindo

Ommystylish kufanya usahili wa model wa kike na wa kiume

Tarehe June 9, 2017

Mkurugenzi wa Ommystylish Campany, Omary Rashidi, akizungumnza na Wanahabari Jijini dar es salaam

Mkurugenzi wa Ommystylish Campany, Omary Rashidi, akizungumnza na Wanahabari Jijini Dar es salaam.

Ommystylish Campany kwa kushirikiana na makampuni mbalimbali ya mitindo nchini Tanzania Wanatarajia kufanya Usahili wa model wa kike na wa kiume mnamo juni 17 jijini Dar es salaam

Akizungumnza na mtandao huu leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Ommystylish Company Omary Rashidi, amesema kuwa usahili huo utafanyika juni 17 kwanzia saa kumi na mbili jioni na kuendelea.

Usahili huo rasmi utafanyika katika hoteli ya Star City Hotel iliyopo maeneo ya Sinza Afrikasana kuanzia saa kumi na mbili jioni na kuendelea mpaka majogoo bila kiingilio chochote.

Rashidi  amewaomba wavulana  na wasichana mbali mbali katika tasnia ya mitindo kujitokeza kwa wingi kujiunga katika usahili huo utakaofanyika siku hiyo kwa ili  kuinua tasnia ya sanaa katika mitindo mbalimbali.

Usahili huo utaburudishwa na wasanii mbalimbali wa kizazi kipya na ngoma mbalimbali za kitamaduni zilizo bobea katika uafrika na tamaduni nyingine za nje ya nchi.

Mkurungenzi wa Ommystaylish, (katikati) Omary Rashidi, kulia ni Mercy Mbelwa, kushoto ni Mariam Mirambo. wakiteta jambo. jijini dar es salaam

Mkurungenzi wa Ommystaylish, (katikati) Omary Rashidi, kulia ni Mercy Mbelwa, kushoto ni Mariam Mirambo. wakiteta jambo. jijini dar es salaam.

_DSC4946

Picha ya pamoja.

Picha ya pamoja.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni