Mitindo

Ommystylish aja Tamasha la Mavazi la ‘Wahenga’

Tarehe August 7, 2017

G70A2456

Mkurugenzi  wa  Ommy Staylish  Company  akizungumnza na Wanahabari Jijini Dar es salaam.

Mwanamitindo anayekuja kwa kasi nchini Tanzania Ommystylish amekuja  na staili mpya ya Wahenga fashion show itakayofanyika ndani ya mji kasoro bahari  Morogoro.

G70A2413

Akiongea na mtandao huu Ommy amesema umefika wakati wa  kutambua umuhimu wa vazi la asili kutoka katika makabila mbalimbali ya hapa nchini.

“Pengine watu hawatonielewa lakini ni vyema kuwakumbusha tulipotoka ili kuenzi asili yetu kwani mitindo bora yenye kuthamini vya kale na kuvienzi hivyo hatuna budi kurudisha heshima ya wahenga”Alisema Ommy.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi Social Education and merry queen technology kuanzia saa saba mchana na mgeni rasmi ni mbunge wa Morogoro mjini mhe. Abood.

Ommy amewaalika Wakazi wa Morogoro na Viunga vyake kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo kwa kiingilio cha shilingi lefu 5.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni