Mitindo

Mkenya atwaa taji la malkia wa urembo Afrika

Tarehe November 20, 2017

Shindano la malkia wa urembo duniani la 2017 limekamilika mjini Sanya China siku ya Jumamosi huku Mkenya Magline Jeruto akishinda taji la malkia wa urembo barani Afrika.

Mwanadada huyo kutoka eneo la Elgeyo Marakwet nchini Kenya amechukua nafasi ya tano katika mashindano hayo. Taji la malkia wa urembo duniani lilichukuliwa na mwanadada wa India Manushi Chhillar.

Andrea Meza wa Mexico alichukuwa nafasi ya pili akifuatiwa na Muingereza Stephanie Hill huku naye Aurore Kichenin wa Ufaransa akishinda nafasi ya nne.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni